http://projects.voanews5aitmne6gs2btokcacixclgfl43cv27sirgbauyyjylwpdtqd.onion/boko-haram-terror-unmasked/how-this-story-was-reported/swahili.html
Ndani, kwa makini zilifungwa kwa karatasi kadhaa za plastiki, kulikuwa na hard drive ndogo. Ilikuwa na zaidi ya mafaili 400 ya video — kitu ambacho kiligeuka na kuwa ni saa 18 za rekodi. Ukiangalia video chache, mwandishi ameshangazwa: Watu katika video walikuwa wapiganaji wa Boko Haram, moja ya makundi mabaya sana na yenye usiri mkubwa duniani.